1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais George W. Bush asaini sheria ya kutatanisha ya kupambana na ugaidi

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1n

Rais wa Marekani, George W. Bush, amesaini sheria ya kupambana na ugaidi ambayo inawaruhusu wachunguzi kutumia mbinu ngumu katika kuwahoji watuhumiwa. Sheria hiyo ya kutatanisha, inairuhusu serikali kuwafungulia mashtaka haraka hata kabla ya halmashauri za kijeshi kushughulikia faili za watuhumiwa hao. Rais Bush amesema sheria hiyo itasaidia kuyalinda maslahi ya Marekani.

Sheria hiyo imekuja baada ya mwezi moja na nusu rais Bush kukiri kuwa shirika la upelelezi la Marekani, CIA, liliwahoji watuhumiwa wa ugaidi wanaozuwiliwa katika nchi za nje. Bush aliliomba baraza la Congres liliidhinishe sheria hiyo bila kupoteza muda wakati ambapo korti kuu ya nchi iliitupilia mbali.