WASHINGTON: Rais George W. Bsuh asema vita nchini Irak ni sawa na vile vya Vietnam | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Rais George W. Bsuh asema vita nchini Irak ni sawa na vile vya Vietnam

Rais wa Marekani George W.Bush, amesema machafuko yanaoikumba Irak yanalingana na yale yaliotokea katika vita vya Vietnam. Hata hivyo, Bush amesema Marekani haina mpango wa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Irak japokuwa waasi wanajaribu kusababisha hasara kubwa ili wanajeshi hao wa kigeni warudishwe nyumbani. Jana maafisa wa kijeshi wa Marekani nchini Irak, waliarifu kuhusu mauaji ya wanajeshi wengine 11 na kupelekea idadi ya wanajeshi kutoka Marekani waliouawa mnamo mwerzi huu kuwa 69.

Kwa upande mwingine nchini Marekani, mahakama ya kijeshi imeanza kusikiliza kesi za wanajeshi wananne wanaotuhumiwa kuhusika katika matukio mawili ya mauaji ya raia nchini Irak. Wawili kati ya watuhumiwa hao wanakabiliwa na hatari ya adhabu ya kifo kuhusu mauaji ya msichana moja waliomuuwa baada ya kumbaka pamoja na familia yake yote.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com