1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais Bush amteua John Bolton kuwa balozi wa Marekani kwa umoja wa mataifa

1 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEoq

Rais George W Bush wa Marekani amemteua John Bolton hii leo kuwa balozi wa Marekani wa umoja wa mataifa. Rais Bush amechukua uamuzi huo hata licha ya bunge la senate kumkataa Bolton, likisema kuchaguliwa kwake kutaiharibia sifa Marekani.

Bush amesema nafasi hiyo ni muhimu kiasi kwamba haiwezi kuendelea kubakia wazi, hususan wakati huu ambapo mazungumzo ya kulifanyia marekebisho baraza la usalama la umoja wa mataifa yanaendelea na Marekani ikiwa vitani.