WASHINGTON: Mwanajeshi wa Kimarekani akutikana na hatia ya ubakaji na mauaji | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Mwanajeshi wa Kimarekani akutikana na hatia ya ubakaji na mauaji

Mwanajeshi wa Kimarekani aliekutikana na hatia ya ubakaji na mauaji ya msichana wa Kiiraqi wa miaka 14 pamoja na mauaji ya familia ya msichana huyo, amepewa adhabu ya kifungo cha miaka 110.

Mahakama ya kijeshi mjini Kentucky,Marekani imemuadhibu Jesse Spielman alie na miaka 23,baada ya kukutikana na hatia ya ubakaji,kupanga njama ya kubaka na makosa 4 ya mauaji.

Waendesha mashtaka wa kijeshi,hawakusema kuwa Spielman alishiriki katika ubakaji au mauaji, lakini wamesema,alikwenda kwenye nyumba ya marehemu,akifahamu kile ambacho wenzake walipanga kufanya na yeye akatumika kama mlinzi.Uhalifu huo ulitokea mwezi Machi mwaka 2006 katika mji wa Mahmudiya,kusini ya Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com