1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mswada wa Demokrats washindwa katika Seneti

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIg

Seneti ya Marekani imeukataa mswada uliopendekeza kupanga tarehe ya kuviondosha vikosi vya Kimarekani kutoka Irak.Wademokrats katika Seneti walishindwa kupitisha sheria hiyo baada ya kuungwa kwa kura 50 na kupingwa kwa 48.Sheria hiyo ingeamrisha kuondosha vikosi vya Marekani kutoka Irak ifikapo Machi mwaka 2008.Rais George W.Bush alitishia kutumia kura ya veto kuupinga mswada huo pindi ungepata kura 60 zilizohitajiwa iliwa kuweza kupitisha sheria hiyo.Mwezi uliyopita,Baraza la Wawakilishi la Marekani, lilipitisha azimio lisilo na uzito wa kutekelezwa,ambalo lilipinga mpango wa serikali wa kutaka kupeleka wanajeshi wengine 21,500 nchini Irak.