1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mshukiwa wa kwanza afikishwa mahakamani

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNH

Mashtaka ya ugaidi yamewasilishwa dhidi ya manamume wa Australia ambaye amekuwa akizuiliwa katika jela ya Guantanamo Bay nchini Cuba kwa kipindi cha miaka mitano.

David Hicks, raia wa Australia aliyesilimu, ni mtuhumiwa wa kwanza wa ugaidi kufikishwa mahakamani kutumia mfumo mpya wa mahakama za kijeshi za Marekani.

Wizara ya ndani ya Marekani inadai Hicks alitoa misaada iliyotumiwa kwa ugaidi kabla kutiwa mbaroni nchini Afghanistan mnamo mwaka wa 2001.

Wakili wa maswala ya kijeshi wa Marekani anayemtetea David Hicks, Michael Mori, ameyakosoa mashtaka mapya, akisema hayajakuwepo katika sheria zinazohusu vita.

Kesi ya David Hicks imeharibu uhusiano baina ya Marekani na mshirika wake Australia. Kesi ya Hicks inatarajiwa kusikilizwa katika kipindi cha miezi minne ijayo.