1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Msaada baada ya kutimizwa masharti yote

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRb

Licha ya Wapalestina kuanza kuunda serikali ya umoja wa kitaifa,Marekani imesema,itaanza kutoa msaada wake baada ya kuona kuwa masharti yote yametimizwa.Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice amesema,hadi hivi sasa hakusikia cho chote ikiwa serikali mpya ya Wapalestina itatambua kuwepo kwa taifa la Israel,itaacha matumizi ya nguvu na kukubali mapatano yaliokuwepo.Siku ya Alkhamisi rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah, alimkabidhi Ismail Haniyeh,madaraka ya kuunda serikali mpya katika muda wa majuma matano. Haniyeh aliekuwa waziri mkuu katika serikali iliyokuwa ikiongozwa na Hamas,alijiuzulu pamoja na wenzake siku ya Alkhamisi,ili kufungua njia ya kuunda serikali mpya itakayokuwa na wajumbe wa Hamas na Fatah.