1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mkutano kuhusu maangamizi makuu wakosolewa

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkw

Marekani imekosoa vikali mkutano uliopangwa kufanywa nchini Iran kuhusu maangamizi makuu.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, mkutano huo si kingine isipokuwa kuwapatia jukwaa wale wanaobisha ukweli wa maangamizi makuu. Ikaongezea kuwa mkutano huo utakaoanza siku ya Jumatatu,ni kitendo kingine cha aibu cha serikali ya Teheran,kuhusika na mauaji ya Wayahudi yaliyofanywa na Wanazi.Hata serikali ya Ujerumani imelalamika kuhusu mkutano huo na mjumbe wa kibiashara katika ubalozi wa Iran aliitwa kwenye ofisi ya wizara ya nje ya Ujerumani mjini Berlin.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Iran,wajumbe kutoka nchi 30 watahudhuria mkutano huo,ikiwa ni pamoja na wajumbe kutoka Ujerumani, lakini chama cha kizalendo cha cha mrengo wa kulia-NPD hakitowakilishwa.