WASHINGTON : Matibabu ya wanajeshi majeruhi kuchunguzwa | Habari za Ulimwengu | DW | 04.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Matibabu ya wanajeshi majeruhi kuchunguzwa

Rais George W. Bush wa Marekani amesema ataunda tume kuangalia upya huduma ya matibabu inayotolewa kwa wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa.

Hatua yake hiyo inakuja baada ya Katibu wa masuala ya jeshi Francis Harvey kulazimishwa kujiuzulu kutokana na repoti kwamba wanajeshi waliojeruhiwa nchini Iraq au Afghanistan wamekuwa wakipatiwa matibabu ya kiwango cha chini.

Wiki iliopita gazeti la Washington Post lilielezea juu ya hali katika Kituo cha Matibabu cha Kijeshi cha Walter Reed mjini Washington ambapo limesema wanajeshi waliojeruhiwa wamekuwa wakipatiwa matibabu kwenye majengo yaliokuwa yamejaa panya na mende.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com