1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mashambulio dhidi ya majeshi ya Marekani Irak yaongezeka Irak

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCi9

Kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya ulinzi ya Marekani, mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Irak yameongezeka kwa asilimia 22.

Ripoti hiyo imelitaja jeshi la Mehdi la shehe wa kishia Moqtada al Sadr kama kundi hatari zaidi kwa usalama wa Irak na linalochochea machafuko ya kikabila nchini humo. Ripoti imesema kuna ongezeko la idadi ya raia wanaouwawa au kujeruhiwa na kulinganisha hali hii na ongezeko la makundi ya mauaji yanayosaidiwa na baadhi ya maofisa wa vikosi vya usalama vya Irak.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates anasubiri ushauri vipi atakavyoendelea kukabilia na hali nchini Irak. ´Nasubiri kusikia tathimini yao ya hali halisi nchini Irak na pia ushauri wao kuhusu vipi tutakavyoendelea katika majuma na miezi ijayo.´