WASHINGTON : Marekani yahitaji muda zaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 10.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Marekani yahitaji muda zaidi

Mabingwa Stuttgart watamba upya ?

Mabingwa Stuttgart watamba upya ?

Marekani imesema inahitaji muda zaidi kuangalia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kati ya makundi ya Wapalestina ili kuyakinisha iwapo yanakidhi masharti ya mataifa ya magharibi ya kurudisha tena msaada wake kwa serikali ya Palestina.

Makubaliano hayo kati ya kundi la Fatah lilnaloungwa mkono na Marekani na Hamas linaloongoza serikali ya Palestina yamefikiwa katika mji mtakatifu wa Mecca nchini Saudi Arabia hapo Alhamisi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani Dane Perino amesema mjini Washington kwamba Marekani inatumai makubaliano hayo yatasaidia kukomesha umwagaji damu kati ya wafuasi wa Fatah na Hamas ambao umepelekea kuuwawa kwa watu 100 tokea mwezi wa Desemba.

Maafisa waandamizi wa Hamas wamesema licha ya kufikiwa kwa makubaliano hayo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katu hawatoitambuwa Israel na wala kujifunga na makubaliano ya amani yaliopo hivi sasa kati ya Israel na Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com