1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani kutuma wanajeshi zaidi Iraq.

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfb

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa itatuma kiasi cha wanajeshi wengine 3,300 nchini Kuwait mapema mwezi wa Januari kuchukua nafasi ya jeshi lililoko mstari wa mbele ambalo limewekwa nchini Iraq.

Jeshi la Marekani linakuwa na wanajeshi wa akiba nchini Kuwait kwa ajili ya kuwabadilisha haraka wanajeshi walioko ndani ya Iraq ama katika eneo lolote la hatari katika eneo hilo kama litahitajika.

Rais wa Marekani George W. Bush anatarajiwa kutangaza mwezi wa Januari mkakati mpya wa nchi yake nchini Iraq ambao unaweza kujumuisha kuimarisha jeshi lililoko hivi sasa, lenye wanajeshi 130,000 kwa kiasi cha wanajeshi wapya wapatao 15,000 hadi 30,000.