1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Kundosha sasa vikosi vya Marekani kutazidisha machafuko Irak

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsJ

Kamanda wa majeshi ya Marekani katika Mashariki ya Kati amepuuza miito iliyotolewa na wanachama mashuhuri wa Demokrat kuviondoa vikosi vya Marekani kwa awamu kutoka Iraq.Jemadari John Abizaid alipotoa ushahidi mbele ya Kamati ya Huduma za Kijeshi ya Baraza la Seneti amesema, anaamini kuwa hatua ya kuviondosha vikosi itasababisha machafuko zaidi nchini Irak.Yeye ametetea mkakati wa hivi sasa wa Marekani kuvisaidia vikosi vya Kiiraki kubeba dhamana ya kudhibiti usalama.