WASHINGTON: Kamati ya bunge yapiga kura dhidi ya mkakati wa Rais George W Bush nchíni Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Kamati ya bunge yapiga kura dhidi ya mkakati wa Rais George W Bush nchíni Iraq.

Kamati ya bunge ya uhusiano wa kimataifa nchini Marekani, imepinga mpango wa Rais George W Bush kupeleka vikosi vya ziada nchini Iraq.

Kamati hiyo imepiga kura kumi na mbili kwa tisa kwa azimio linaloeleza mkakati mpya wa Rais George W. Bush kuwa hautaifaidisha Marekani kwa vyovyote vile.

Kamati hiyo imetoa wito wa kuandaliwa taratibu za kuikabidhi usalama serikali ya Iraq.

Kamati hiyo imepiga kura siku moja baada ya Rais George Bush kulihutubia bunge na kutoa wito wa kuungwa mkono mkakati wake mpya nchini Iraq.

Kwenye hotuba yake hiyo ya kwanza kwenye bunge linalodhibitiwa na chama cha Demokratic, Rais Bush alitahadharisha endapo Iraq itashindwa kupata amani, eneo zima la Mashariki ya Kati litaathirika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com