1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Jeshi la Marekani lawasaka wanamgambo wa mahakama za kiislamu wa Somalia

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdU

Jeshi la wanamaji la Marekani limejiunga na juhudi za kuwasaka wanamgambo wa mahakama za kiislamu waliotimuliwa kutoka Somalia wakiwatuhumu kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaeda.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Marekani, Sean McCormack, amesema wanajeshi wa Marekani walio nchini Djibouti wanashika doria katika pwani ya Somalia wakiwatafuta viongozi wa mahakama za kiislamu na washukiwa wa kundi la al-Qaeda, waliofanya mashambulio ya mabomu dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mnamo mwaka wa 1998.

Aidha McCormack amesema Marekani inashirikiana kwa karibu na mataifa jirani na Somalia kuhakikisha washukiwa hao hawavuki mipaka na kuingia nchi hizo. Hata hivyo hakusema ni wanajeshi wangapi wa Marekani wanaoshiriki katika operesheni hiyo.