WASHINGTON : Gates amtaarifu Rais Bush juu ya ziara yake | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Gates amtaarifu Rais Bush juu ya ziara yake

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates jana amekuwa na mazungumzo na Rais George W . Bush huko Camp David Maryland.

Mazungumzo yao yamelenga juu ya ziara ya waziri huyo wa ulinzi nchini Iraq wiki hii.Rais Bush anatarajiwa kujadili suala hilo la Iraq na timu yake ya usalama wiki ijayo.Msemaji wa Bush amesema hapo mapema kwamba rais ameridhishwa na hatua inayopigwa katika kusanifu sera mpya ya Iraq.

Katika hotuba yake ya mwisho kwa taifa kwa njia ya radio mwaka huu Rais Bush amewashukuru wanajeshi wa Marekani walioko Iraq kwa juhudi zao na amesema ataendelea kuwaunga mkono katika kipindi cha usoni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com