1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Gates aidhinishwa kuwa waziri wa ulinzi

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCls

Baraza la Senate la bunge la Marekani limemuidhinisha mshauri wa muda mrefu wa rais Robert Gates kuwa waziri mpya wa ulinzi kuchukuwa nafasi ya Donald Rumsfeld ambaye amejiuzulu mwezi uliopita baada ya chama cha Republican cha Rais George W. Bush kupoteza udhibiti wa bunge.

Kura za ndio zilikuwa 95 dhidi ya mbili.Uteuzi huo wa Gates uliidhinishwa kwa kauli moja na Kamati ya Huduma za Kijeshi ya baraza la Senate hapo jana.Akizungumza wakati wa kikao cha kuthibitishwa kushika wadhifa huo Gates amewaambia wajumbe wa kamati hiyo kwamba alikuwa haamini kuwa Marekani ilikuwa inashinda vita nchini Iraq na pia ameonya kwamba vita hivyo vinaweza kulitumbukiza vitani eneo zima la Mashariki ya Kati.