1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush kukutana na Putin

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmf

Rais wa Urusi, Vladamir Putin, yumo nchini Marekani kwa mazungumzo na rais George W Bush.

Mazungumzo yao leo yanatarajiwa kutuwama juu ya hali ya wasiwasi iliyopo baina ya Marekani na Urusi. Mahusiano baina ya nchi hizo mbili yameathiriwa na mpango wa Marekani kutaka kujenga mfumo wa ulinzi wa makombora mashariki mwa Ulaya na kutokubaliana kuhusu hatima ya jimbo la Kosovo nchini Serbia.

Marekani na Urusi zimeyaeleza mazungumzo hayo kuwa yasiyo rasmi na kufutilia mbali uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya maana.

Wakati huo huo, maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kupinga mkutano baina ya rais Bush na rais Putin karibu na eneo wanakokutana viongozi hao mjini Kennebunkport kaskazini mashariki mwa Marekani.

Maandamano hayo yamelenga kupinga hatua ya Marekani kujihusisha na vita vya Irak.