WASHINGTON : Bush kukutana na Abbas | Habari za Ulimwengu | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Bush kukutana na Abbas

Rais George W. Bush wa Marekani anatazamiwa kukutana na Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina mjini New York pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo Jumatatu.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema viongozi hao wawili wataendelea na mazungumzo kuhusu suluhisho la kuwa na mataifa mawili katika mzozo wa Mashariki ya Kati.Bado haiko wazi iwapo Bush pia atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert mjini New York wakati wa kikao hicho cha Umoja wa Mataifa.

Tangazo hilo linafuatia mfululizo wa mazungumzo wiki hii kati ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice na Abass na Olmert.

Mazungumzo hayo yalikuwa yamekusudia kukamilisha mipango ya mkutano wa amani unaodhaminiwa na Marekani uliopangwa kufanyika baadae mwaka huu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com