1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush kuelezewa mikakati mbadala nchini Iraq.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgt
Mkutano wa Waislamu uliwavutia waandishi habari
Mkutano wa Waislamu uliwavutia waandishi habariPicha: picture-alliance/dpa

Waziri mpya wa ulinzi wa Marekani Robert Gates anatarajiwa leo kumfahamisha rais George W. Bush kuhusu mwelekeo mpya kuhusiana na vita nchini Iraq.

Gates amerejea kutoka katika ziara katika eneo la vita yenye lengo la kutafuta mkakati mbadala kuweza kupambana na hali ya machafuko na kuweza kuruhusu majeshi ya Marekani kurejea nyumbani.

Gates amekataa kutoa maelezo ya mkakati huo ambao anajaribu kuukamilisha pamoja na makamanda wake , lakini amewashutumu viongozi wa kisiasa wa Iraq pamoja na kutaka wachukue jukumu kwa ajili ya usalama wa nchi hiyo.

Jeshi la Marekani limeripoti kuwa wanajeshi wake watano wameuwawa nchini Iraq wakati wa ziara ya waziri huyo nchini humo.