1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush hatotia saini mswada kuwa sheria

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFa

Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani limepiga kura kupanga tarehe 31 mwezi Agosti mwaka 2008,kuondosha vikosi vya Marekani kutoka Irak.Baraza hilo linalodhibitiwa na chama cha Demokrat,limepitisha mswada kwa kura 218 dhidi ya 212.Hatua hiyo inatazamwa kama ni changamoto kali kwa sera za vita za Rais George W.Bush.Baraza la Seneti la bunge la Marekani,linatazamiwa pia kupiga kura juma lijalo,lakini rais Bush alipozungumza na waandishi wa habari mjini Washington alisema yeye,hatotia saini mswada huo kuwa sheria.