1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush awashambulia wakosoaji wake.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCao

Rais wa Marekani amewashambulia wakosoaji wa mkakati wake mpya kuielekea Iraq na kusema watoe mkakati wao wa kusitisha ghasia mjini Baghdad.

Katika hotuba yake kwa njia ya radio kila wiki, Bush amesema kuwa mpango wake umeweka dhamana kwa serikali ya Iraq kuchukua jukumu la usalama na kufikia maridhiano ya kisiasa.

Hapo mapema wiki hii ametangaza kuwa anania ya kutuma wanajeshi 21,000 zaidi wa Marekani nchini Iraq.

Wabunge wa chama cha Democratic katika bunge la nchi hiyo wanataka kupeleka katika kikao cha bunge muswada utakaopinga kuongezwa kwa majeshi ya Marekani na wanamatumaini ya kupata kura nyingi kutoka kwa wabunge wa chama cha Republican na kumtenga Bush.

Katika ishara ya nia yake ya kupata uungwaji mkono katika chama chake, Bush alifanya mikutano na wabunge kadha waandamizi wa chama cha Republican katika sehemu ya mapumziko ya rais huko Camp David.