1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush atakutana na viongozi wa Washia na Wasunni

2 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnU

Duru za Ikulu ya Marekani zinasema,wajumbe wa Washia na Wasunni wanaohasimiana,watakutana na rais wa Marekani George W.Bush.Majadiliano ya kwanza yanatazamiwa kufanywa siku ya Jumatatu pamoja na Mshia mwenye usemi mkubwa,Abdel Aziz al-Hakin,wa Muungano wa vyama vya Kishia wenye viti 128 katika bunge la Irak.Na Januari ijayo, Bush amepanga kukutana na makamu wa rais wa Irak,Tareq al-Hashimi alie Msunni.Mikutano hiyo imepangwa baada ya Bush na waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki kukutana nchini Jordan siku ya Alkhamisi kwa azma ya kutafuta njia ya kukomesha machafuko nchini Irak.Nchi hiyo ipo katika hatari ya kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya mapigano makali,kati ya wanamgambo wa Kishia na Wakisunni.Mapigano hayo yakiendelea tangu miezi kadhaa,yanasababisha mmuagiko mkubwa wa damu nchini Irak.