WASHINGTON: Bush amekiri uwezekano wa kufuata njia mpya | Habari za Ulimwengu | DW | 09.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Bush amekiri uwezekano wa kufuata njia mpya

Rais George W.Bush wa Marekani amekiri kuwa huenda ikawa njia mpya inahitaji kufuatwa kusuluhisha mgogoro wa Irak.Baada ya kukutana na viongozi wa Baraza la Congress mjini Washington, Bush alisema atashirikiana na pande zote zilizohusika kutafuta njia ya kufuatwa.Wakati huo huo,gazeti la Washington Post linaripoti kuwa serikali ya Bush inachunguza mikakati mitatu mbali mbali,ikiwa ni pamoja na kuongeza kwa muda mfupi,idadi ya vikosi vya Kimarekani hadi 30,000 kusaidia kuleta usalama katika mji mkuu wa Irak Baghdad pamoja na kutoa mafunzo kwa vikosi vya Kiiraki.Mkakati mwingine,unashauri kuwa vikosi vya Kimarekani vishughulike zaidi kuwasaka wale wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la al-Qaeda na mkakati wa tatu unashauri kuimarisha msaada wa kisiasa wa Marekani kwa vyama vya Washia walio wengi.Kwa upande mwingine waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier,akiwa ziarani mjini Washington alisema,sasa ni mapema mno kwa Ujerumani kutamka ikiwa itachukua dhima kubwa zaidi ya kidplomasia kusaidia kusuluhisha mgogoro wa Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com