1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Bush akana mauaji ya kimbari ya Warmenia

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7I3

Rais George W. Bush wa Marekani amekataa pendekezo la wabunge kuyaainisha rasmi mauaji na kupotezewa makaazi kwa Waarmenia kati ya mwaka 1915 na mwaka 1918 kuwa ni mauaji ya kimbari.

Bush ametowa uamuzi huo baada ya kuzungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayip Erdogan.

Takriban Waarmenia milioni 1 na nusu inaaminika kuwa wameuwawa wakati Himaya ya Ottoman ya Uturuki iliposambaratika.

Uturuki inasema idadi ya Waarmenia waliouwawa kuwa ni pungufu ya theluthi moja na inakanusha kwamba hayo yalikuwa ni mauaji ya kimbari.