WASHINGTON : Bush aionya Korea Kaskazini | Habari za Ulimwengu | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Bush aionya Korea Kaskazini

Rais George W. Bush wa Marekani ameionya Korea Kaskazini dhidi ya kuipatia Syria maarifa ya nuklea kwa kusema kwamba mazungumzo ya pande sita na serikali ya Korea Kaskazini yanaweza tu kufanikiwa iwapo itatimiza ahadi zake zote.

Hata hivyo duru mpya ya mazungumzo iliokuwa imepangwa kufanyika hapo Jumaatano iliahirishwa ghafla kutokana na kuwepo kwa repoti kwamba serikali ya Korea Kaskazini ilikuwa ikisaidia Syria kutengeneza silaha za nuklea.

Serikali zote mbili za Korea Kaskazini na ile ya Syria zimekanusha repoti hizo.Katika makubaliano ya kihistoria yaliofikiwa hapo mwezi wa Februari utawala wa kikomunisti wa Korea Kaskazini ulikubali kutokomeza mitambo yake yote ya nuklea na mipango ili badala yake nchi hiyo ipatiwe ridhaa za kidiplomasia nishati pamoja na msaada mwengine.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com