Washington. Bush aahidi kushirikiana na Wademocrats. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. Bush aahidi kushirikiana na Wademocrats.

Katika hotuba yake ya kila wiki kwa njia ya radio, rais wa Marekani George W. Bush ametoa kwa viongozi wa chama cha Democratic kinachodhibiti baraza la Congress ahadi ya ushirikiano katika kupunguza urari katika bajeti na kuimarisha elimu.

Lakini Bush ameamua kabisa kukwepa suala la vita vya Iraq, ambalo linatishia kuingia katika mapambano makubwa ya kisiasa katika wiki zijazo.

Viongozi wa chama cha Democratic wamemwandikia barua Bush siku ya Ijumaa, wakimtaka kutoongeza wanajeshi nchini Iraq na kumaliza vita hivyo vya Iraq.

Bush anatarajiwa kutoa mkakati mpya kwa ajili ya Iraq wiki ijayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com