WASHINGTON: Bunge lapitisha mswada kupiga vita ugaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 28.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Bunge lapitisha mswada kupiga vita ugaidi

Bunge la Marekani limeptisha mswada wa sheria kuhusika na njia za kupiga vita ugaidi.Mswada huo,unafungamanisha baadhi kubwa ya mapendekezo yaliotolewa na halmashauri iliyoundwa kuchunguza mashambulizi ya Septemba 11.Miongoni mwa hatua mpya za usalama,ni kuanzishwa kwa utaratibu wa kukagua shehena zote,kabla ya kupakiwa katika ndege za abiria au meli.Hatua za usalama pia zitaimarishwa kwenye bandari na viwanja vya ndege.Na miji inayokabiliwa zaidi na vitisho vya kigaidi,itapewa misaada zaidi ya pesa,kuboresha ulinzi wa usalama.Mswada huo sasa umepelekwa kwa Rais George W.Bush kutiwa saini,ili uweze kuwa sheria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com