WASHINGTON : Afrika yapiga hatua dhidi ya umaskini | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Afrika yapiga hatua dhidi ya umaskini

Benki ya Dunia imesema Afrika inapiga hatua dhidi ya umaskini lakini jambo hilo linakwamishwa na ukosefu wa matumizi ya kutosha kwa miundo mbinu.

Uwekezaji kwenye miradi kama vile ya barabara,vinu vya umeme na bandari unatakiwa uongezeke maradufu kufikia euro bilioni 16 kwa mwaka.Venginevyo Afrika itashindwa kufikia Malengo yake ya Maendeleo ya Milinia ifikapo mwaka 2015.Benki hiyo ya Dunia pia imeyataka mataifa ya kitajiri kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kuisaidia Afrika na imekadiria kwamba mataifa yenye utajiri wa mafuta barani Afrika yatakuwa yamejipatia mapato ya euro bilioni 160 kati ya mwaka 2000 na mwaka 2010.

Kwa upande mwengine Benki ya Dunia imesema viwango vya kuandikishwa watoto katika shule za msingi vimeongezeka barani kote Afrika na viwango vya vifo vya watoto wachanga imeanza kupunguwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com