Waserbia wapiga kura kuchagua bunge | Habari za Ulimwengu | DW | 11.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Waserbia wapiga kura kuchagua bunge

-

BELGRADE

Wananchi wa Serbia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa mapema wa bunge ambao unatazamiwa kuwa ni muamuzi juu ya mustakabala wa sera za nje za taifa hilo la Balkan.Kura za maoni zinaonyesha kwamba utakuwa mpambano mgumu kati ya chama chenye msimamo mkali cha nationalist Radical Party na Demokratic Party cha rais Boris Tadic.Chama cha msimamo mkali ambacho kiongozi wake wa zamani Vojislav Seseji anashtakiwa kwa uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague kinawania uchaguzi huo chini ya mwelekeo wa kupigia debe mafungamano ya karibu zaidi na Urussi. wakati wademokrats wanataka kuilekeza Serbia katika kujiunga na Umoja wa Ulaya.Uchaguzi huu wa mapema umeitishwa baada ya kuvunjika kwa serikali ya muungano wa chama cha Waziri mkuu Vojislav Kostunica cha Demokratic Party of Serbia na Demokratic Party.Muungano huo ulivunjika baada ya nchi nyingi za Umoja wa Ulaya kuutambua uhuru wa jimbo lililojitenga na Serbia la Kosovo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com