Wasanii watakaohudhuria uapisho wa Biden-Harris
Bruce Springsteen na Lady Gaga ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza hafla ya kuapishwa Joe Biden na makamu wake. Ifuatayo ni orodha ya wasanii wengine watakaohudhuria.
Lady Gaga
Mwaka huu hakutokuwa na umati kushuhudia tukio hilo kutokana na janga la virusi vya corona pamoja na wasiwasi wa usalama hasa baada ya uvamizi uliofanywa kwenye majengo ya bunge mapema mwezi Januari. Biden ataapishwa katika hafla ya watu kidogo. Lady Gaga atatumbuiza kwa kuimba wimbo wa taifa
Jennifer Lopez
J.LO pia amepangwa kutumbuiza wakati wa hafla ya kuapishwa. Mwanamuziki huyo amekuwa wazi kuunga mkono Democratic, alipopiga picha mara baada kupiga kura na kuwashirikisha timu ya Biden. Kulingana na kamati ya maandalizi, uwepo wa wasanii tofauti kunatoa taswira ya uwakilishi wa kila mtu katika taifa hilo kubwa.
Bruce Springsteen
Joe Biden atakuwa ni rais wa 46 wa Marekani kuanzia Januari 20, lakini mwaka huu hafla kubwa itakuwa ni kupitia televisheni, iliyopewa jina la "kusherehekea Marekani". Itawashirikisha wanamuziki akiwemo Bruce Springsteen ambaye wimbo wake wa "Born in USA" ni kama wimbo wa taifa na mara nyingi ametumbuiza kwenye uteuzi wa Democtrats.
Jon Bon Jovi
Msanii mwingine mashuhuri wa Rock ni Jon Bon Jovi. Kama ilivyo kwa Springsteen na wengine wengi watakaojitokeza kwenye tukio hilo kubwa, pia amekuwa mkosoaji wa Donald Trump. Rais Trump hakuwa na umaarufu katika tasnia ya Hollywood, wasanii wengi wakubwa waligoma kutumbuiza wakati wa sherehe za kuapishwa kwake na baadhi ya wasanii hata walifungua mashitaka kwa kutumia nyimbo zao kwenye kampeni.
John Legend
John Legend awali alitangaza kumuunga mkono mgombea wa Democratic kwa kujitokeza katika mikutano ya Kamala Harris mwezi Novemba 2020. Pia wamo Justin Timbarlake na muimbaji Demi Lovato.
Eva Longoria
Kerry Washington na Eva Longoria watawakilisha upande wa wasanii wa uigizaji. Longoria, ambaye alijipatia umaarufu katika kipindi cha televisheni cha "Desperate Housewives," si mgeni katika kuhudhuria matukio ya chama cha Democratic na hata kampeni zake. Alimpigia kampeni Biden na Harris huko Florida
Tom Hanks
Mwigizaji huyu mkongwe ndiye ataongoza tukio hili la dakika 90 kwenye TV ambalo limepangwa kuwatunuku mashujaa wa kila siku ambao ni raia wa Marekani, akiwemo dereva wa UPS, mwalimu wa chekechea na Sandra Lindsay, ambaye alikuwa Mmarekani wa kwanza kupatiwa chanjo ya COVID-19 mara baada ya kuidhinishwa.
Lin-Manuel Miranda
Hafla hiyo itajumuisha pia wasanii ambao sio wanamuziki. Lin-Manuel(kushoto) ambaye aliandika na kushiriki kwenye Hamilton ambayo inasimulia maisha ya utotoni ya baba na mwanzilishi wa Marekani Alexander Hamilton, ambaye ataonyesha kazi yake. Wengine ni nyota wa NBA Kareem Abdul-Jabbar.