Waraka wa kimataifa dhidi ya mauwaji ya halaiki | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Waraka wa kimataifa dhidi ya mauwaji ya halaiki

Miaka 60 tangu waraka wa kimataifa dhidi ya mauwaji ya halaiki ulipopitishwa na jumuia ya kimataifa.

Jengo la mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague

Jengo la mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague


Ulikua waraka wa kwanza wa kimataifa ambao walimwengu walilazimika kuuheshimu-waraka wa kuhifadhi haki za binaadam.Na miaka 60 baadae,waraka huo bado ni muhimu,kijamii na kisiasa:Waraka wa kinga na adhabu dhidi ya mauwaji ya halaiki.Mahakama kuu ya kimataifa iliyoundwa tangu mwaka 2003 ndio chombo kinachohakikisha waraka huo unatekelezwa.Na mahakimu wa taasisi hiyo hawajawahi kulalamika dhidi ya uhaba wa mwamko wa kisiasa.Kinachokosekana lakini ni uungaji mkono wa wanasiasa.Hali hiyo inakutikana nchini Marekani,sawa na katika nchi mfano wa Sudan ambako sheria haziheshimiwi.Maneno matupu yakome-anasema mtaalam wa haki za jamii Hans Peter Kaul-hakimu pekee wa kijerumani katika mahakama ya kimataifa mjini The Hague.Jumuia ya kimataifa ilidhihirika imeungana kwa dhati december 9 mwaka 1948,baada ya vita vya kikatili walivyoshuhudia.Kamwe mauwaji ya kikatili ya halaiki kama walivyofanya wanazi dhidi ya wayahudi,hayataachiowa kutokea.Katika enzi za vita baridi,waraka huo haukuweza kutumika.Nani angeweza kukiuka kambi zilizokuweko ili kuhakikisha kama waraka huo unatekelezwa?Ungewakilishwa na nani? Na wahalifu wangepelekwa mbele ya mahakama gani?Ukuta ulipoporomoka na kambi kutawanyika ndipo watu walipofanikiwa,kupitia mahakama ya kimataifa.


Tafsiri ya waraka huo wa Umoja wa mataifa ni bayana:Yanatajwa kua mauwaji ya halaiki,kisa chochote kile kinachofanywa kwa lengo la kutaka kuwaangamiza watu wote kwa jumla au sehemu ya jamii naiwe katika daraja ya kitaifa,kikabila au kidini.


Kama mauwaji yaliyofanywa na Khmer Rouge katika miaka ya sabiini nchini Cambodja,kama yalivyokua mauwaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda mnamo mwaka 1994 na kama ilivyotokea mwaka mmoja baadae,wabosniak elfu nane walipouliwa huko Srebrenica.


Shida inakutikana lakini katika kudhibiti na kukusanya ushahidi.Waraka unayalazimisha mataifa yazuwie mauwaji ya halaiki yasitokee,unayalazimisha mataifa pia yawaadhibu w aahusika pindi yakitokea.Lakini mataifa mengi hayatekelezi majukumu hayo.Ndio maana wanasheria hawajakosea wanapolalamika dhidi ya walakini katika kungwa mkono kisiasa waraka huo.Ni kweli kwamba mahakama maalum imeundwa, yaani mahakama kuu ya kimataifa.Lakini kama serikali hazishirikiani nayo kikamilifu,wahalifu hawakamatwi kama ilivyotajwa ndani ya waraka huo wa Umoja wa mataifa na kufikishwa mahakamani,ndio maana juhudi za kisheria za kuwaandama zinazuwilika na baadhi ya wakati hata kukorofika.Kila wakati mahakama ya kimataifa inapambana na vizingiti kama hivyo.


Mfano nchini Marekani;Utawala wa rais Bush umekua kila kwa mara ukikosoa shughuli za mahakama hiyo kwa namna ambayo mtu anaweza kusema,utawala huo umekua ukisussia shughuli za mahakama ya kimataifa.Hapo rais mteule Obama anaweza kubainisha jinsi anavyothamini muuondo wa sheria unaotilia maanani haki za binaadam.


Yeyote anaejaribu kukwepa kufuata maadili yaliyoshadidiwa ndani ya waraka huo,kimsingi anakiuka pia haki za binaadam.Kama kwa mfano serikali ya Sudan inayoendelea kuwaunga mkono wanamgambo wanaowatimua na kuwatumilia nguvu raia huko Darfour.Maelfu wanayapa kisogo maskani yao kila kukicha.Watu laki tatu wamepoteza maisha yao kutokana na matumizi ya nguvu,njaa na maradhi tangu mzozo huo uliporipuka mnamo mwaka 2003.Yote hayo yanatokea kwasababu serikali inafanya makusudi kuchochea mzozo,na inapalilia propaganda za kikabila kwasababu ya kiu cha kugawana madaraka ya kisiasa.Hiyo ndio maana rais wa Sudan Omar El Bashir ameshitakiwa katika mahakama ya kimataifa kwasababu ya mauwaji ya halaiki na kuhusika na uhalifu dhidi ya ubinaadam .

 • Tarehe 09.12.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GCBQ
 • Tarehe 09.12.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GCBQ
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com