1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Wapiganaji wa itikadi kali waua watu 52 Msumbiji

22 Aprili 2020

Polisi ya Msumbiji imesema kiasi wanakijiji 52 katika jimbo tete la kaskazini ya nchi hiyo la Cabo Delgado waliuwawa na wapiganaji wa itikadi kali mwanzoni mwa mwezi Aprili.

https://p.dw.com/p/3bFIg
Mosambik, Cabo Delgado: Soldat in Naunde
Picha: Borges Nhamire

Kisa hicho ni moja ya matukio mabaya kabisa kuwahi kutokea nchini humo. Rashid Chilumba na maelezo kamili

Msemaji wa polisi ya Msumbiji Orlando Modumane amearifu kuwa wahalifu hao waliwauwa vijana 52 bila kubagua kutokana na hasira baada ya kundi hilo kukataa mipango ya kusajiliwa kuwa wapiganaji wa itikadi kali.

Kulingana na Modumane mauaji hayo yalitokea katika wiliya ya Muidumbe iliyopo jimboni Cabo Delgado, eneo lenye miradi mikubwa ya gesi asilia inayoongozwa na kampuni za kimataifa ikiwamo Total.

Duru kutoka eneo hizo zimearifu kuwa washambuliaaji waliwapiga risasi kichwnai au kuwakata vichwa wale waliouwawa.

Walioshuhudia wamesema siku ya mkasa huo mnamo April 7 washambuliaji walichoama moto vifaa vya ujenzi wa daraja, kuharibu miundombinu ya shule, hospitali na mabenki.

Msako mkali umeanzishwa kuwabaini washambuliaji 

Mosambik, Macomia: Mucojo village had houses destroyed by armed groups
Picha: Privat

Polisi tayari imetangaza msako mkubwa kuwatafuta waliohusika ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Kabla ya kushambulia wahalifu hao walitumia vipaza sauti kuwaonya wanakijiji kutokimbia na badala yake wabakie majumbani.

Taarifa kuhusu kisa hicho zimetolewa wiki moja tangu mkuu wa polisi ya Msumbiji Bernardino Rafael alipopinga madai kwamba sehemu ya jimbo la Cabo Delgado liko chini ya udhibiti wa wapiganaji wa itikadi kali.

Matamshi ya afisa yalifuata kuongezeka kwa mashambulizi yanayovilenga vijiji na majengo ya serikali.

Katika wiki za hvii karibuni wanamgambo wenye silaha wamezidisha mashambulizi kama sehemu ya kampeni yao ya kuanzisha utawala wa kikhalifa katika jimbo la Capo Delgado.

Makundi ya wapiganaji wake yanakamata majengo ya serikali, kuweka vizuizi barabarani na kupeperusha bendera ya rangi nyeusi na nyeupe katika mjini na vijiji vya jimbo hilo.

Hali dhaifu ya usalama inawalazimisha watu kukimbia 

Mosambik Illegale Edelstein-Minen
Picha: DW/E. Valoy

Kwa mujibu wa asasi moja inayofuatilia hali ya mizozo ya kutumia silaha, katika muda wa karibu miaka miwili sasa magaidi kaskazini ya Msumbiji  wamevilenga vijiji vilivyojitenga na kuwauwa zaidi ya watu 900

Hali hiyo imewalazimisha mamia kwa maekfu ya wakaazi kuyahama maakazi na kuongeza wasiwasi kwa kampuni kubwa za kuchimba zinazoendesha shughuli zake kwenye mkoa huo.

Askofu mkuu wa jimbo katoliki katika jimbo la Cabo Delgado amekadiria watu 200,000 wameyatelekeza makaazi ya pembezoni na kutafuta hifadhi kwenye mji wa bandari uitwao pemba ambao ni makao makuu ya jimbo la Delgado.

Tawi la kundi linalojiita dola la kiislamu limedai mara zote kuhusiana na yanayotokea jimboni Cabo Delgado.

Wakati waliposhambulia kwa mara ya kwanza Oktoba 2017, kundi hilo limekuwa likificha utambulisho wake lakini hivi karibuni limewaruhusu wapiganaji wake kuondoa vitambaa vinavyofunika nyuso na na kutangaza hadharani lengo la kuunda utawala unaofuata misingi ya dini ya kiislam kwenye eneo hilo.

Mwandishi: Rashid Chilumba

Mhariri: Iddi Ssessanga