Wapiganaji 11 wa kishia wauawa | Habari za Ulimwengu | DW | 27.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Wapiganaji 11 wa kishia wauawa

BAGHDAD.Majeshi ya Marekani yamewaua wanamgambo 11 wa kishia mapema hii leo huko katika mji wa kusini wa Kut.

Jeshi la Marekani limesema kuwa shambulizi hilo lililengwa kwa wapiganaji wa kundi la Al-Mahdi ambalo ni la kiongozi mwenye msimamo mkali wa kishia Moqtada al Sadri.

Katika harakati nyingine za kupambana na wanamgambo hao, majeshi ya Marekani yamewakamata wapiganaji wawili katika jimbo la Anbar lililoko magharibi wa Iraq.

Katika jimbo la Kaskazini la Nineveh wanajeshi wawili wa Marekani wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa wakati wa mapambano na watu waliyokuwa na silaha.

Vifo hivyo vinafanya idiadi ya askari wa Marekani waliyouawa mapaka sasa toka mwaka 2003 kufikia elfu 3 na mia tisa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com