1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina 2 wauawa katika shambulizi la Israel

23 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DC7a

GAZA:

Wanamgambo 2 wa Kipalaestina wameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyofanywa na vikosi vya Kiisraeli kwenye Ukanda wa Gaza.Ripoti zinasema, wanamgambo hao walikuwa wanachama wa kundi la Al-Quds Brigade ambalo ni tawi la kijeshi la Islamic Jihad.Wakati huo huo,hadi makombora mawili yalirushwa na wanamgambo wa Kipalestina kutoka Gaza na kulenga eneo la kusini ya Israel.Makombora hayo yalianguka katika uwanja ulio tupu karibu na mji wa Sderot na hakuna aliejeruhiwa.Shambulizi hilo limetokea wakati kiasi ya Waisraeli 10,000 kutoka sehemu mbali mbali nchini humo walikuwa wamekusanyika Sderot kuwaunga mkono wakaazi wa mji huo unaoshambuliwa mara kwa mara na maroketi kutoka eneo la Gaza.

Na kwenye Ukingo wa Magharibi kama Wapalestina na wanaharakati 2,000 wa Kiisraeli na nchi za kigeni waliandamana kupinga ukuta wa Israel kwenye kijiji cha Bilín,kilicho kaskazini-magharibi ya Jerusalem katika Ukingo wa Magharibi.