1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanigeria wapiga kura leo

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8O

HABARI KAMILI:

ABUJA:

Wanigeria wameanza kupiga kura hii leo katika uchaguzi wa rais ambao umegubikwa na mabishano makubwa na machafuko.Maafisa wa uchaguzi wakijitahidi kufikisha hati za kupiga kura katika vituo 120.000 hadi dakika ya mwisho.Upigaji kura ulihachelewa kuanza kwa masaa 2.

Taarifa za hivi punde kutoka Abuja,mji mkuu wa Nigeria, zasema, lori la kupakia petroli likiwa na shehena ya gesi lililengwa kuhujumu makao makuu ya Tume ya Uchaguzi ya Nigeria huko Abuja.Lori hilo lilishindwa kuripuka masafa mafupi kutoka jengo hilo.Polisi imerifu, hakuja kuwa na mtu ndani ya lori hilo.Laiti lori hilo lingeifikia shabaha yake,asema msemaji wa polisi Haz Iwendi , alisema basi pangezika mripuko mkubwa.

Matokeo ya uchaguzi huu yanatazamiwa kukabidhi hatamu za utawala kwa mara ya kwanza kutoka rais mmoja wa kiraia kwenda kwa mwengine.Rais wa sasa Olesegun Obasanjo anaeacha madaraka amuungamkono Umaru Yir’Adua.Wagombea wengine ni kiongozi wa zamani wa Nigeria Mohammad Buhari na makamo-rais Atiku Abubakar.