1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanigeria wapiga kura kuchagua rais wao

16 Aprili 2011

Wapiga kura nchini Nigeria wanapiga kura leo hii (16.04.2011)katika uchaguzi wa rais wa taifa hilo ambalo ni la kwanza kwa idadi ya watu barani Afrika. Uchaguzi huu unawakutanisha wagombea wanne.

https://p.dw.com/p/10uZ6
Wapiga kura kwenye jimbo la Kano
Wapiga kura kwenye jimbo la KanoPicha: DW

Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha People's Democratic (PDP) anachuana vikali na Meja Jenerali Mstaafu Muhammadu Buhari wa Congress for Progressive Change (CPC), Nuhu Ribadu wa Action Congress of Nigeria (ACN) na Ibrahim Shekarau wa All Nigeria People's Party (ANPP).

Bango la kituo cha kupigia kura
Bango la kituo cha kupigia kuraPicha: DW/Thomas Moesch

Buhari na Ribadu wanaonekana kutoa upinzani mkali kwa Rais Jonathan, lakini huenda rais huyo akashinda kwa kiwango kidogo. Buhari aliwahi kuwa rais aliyeingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi hapo mwaka 1983 kabla naye kupinduliwa na Jenerali Ibrahim Babangida miaka miwili baadaye.

Ribadu ndiye mgombea kijana kabisa akiwa amezaliwa mwaka 1960, na ndiye aliyekuwa mkuu wa kamisheni ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria, ambayo ilichukua hatua kali dhidi ya mafisadi nchini humo baina ya mwaka 2005 na 2006.

Uchaguzi wa leo unatarajiwa kurejea mafanikio ya uchaguzi wa bunge wa wiki iliyopita, ambao pamoja na matukio ya hapa na pale, umetajwa kuwa ulikuwa mzuri zaidi kulinganisha na chaguzi zilizopita kwenye nchi hiyo.