1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake 23 wafa maji Sudan

Grace Kabogo
4 Aprili 2022

Viongozi wa Sudan wamesema wanawake wapatao 23 wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Mto wa Blue Nile wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/49Qie
Sudan Khartum | Omdurman Brücke
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Shirika la habari la serikali, SUNA limeripoti leo kuwa boti hiyo ilikuwa na watu 29 wakati inazama siku ya Ijumaa kwenye jimbo la Sennar.

Abiria wote walikuwa wanawake, isipokuwa nanodha ambaye amenusurika pamoja na abiria wengine watano. Taarifa hiyo haikuelezea sababu za ajali hiyo.

Kwa mujibu wa SUNA, miili 13 iliopolewa na wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kuitafuta miili mingine 10.

Wanawake hao walikuwa vibarua katika mashamba kwenye eneo la Souki na walikuwa wakirejea nyumbani wakati boti hiyo ilipozama.

Mto wa Blue Nile ni njia muhimu ya watu na bidhaa kwenye taifa hilo la Afrika.