1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasiasa waliokamatwa nchini Kenya waachiwa kwa dhamana

Josephat Nyiro Charo16 Juni 2010

Nchini Kenya Polisi waliwatia nguvuni wabunge watatu na mwanaharakati mmoja wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya Agosti mwaka huu

https://p.dw.com/p/NsUM

Naibu waziri wa barabara Wilfred Machage, Fred Kapondi mbunge wa Mt Elgon, Joshua Kutuny wa Charanganyi na mwanaharakati Christine Nyagitha. Hali mnamo siku za karibuni imekuwa tete kukiwa na mvutano kati ya makundi mawili hata miongoni mwa wanasiasa, kati ya wanaoipinga rasimu ya katiba mpya na wanaoiunga mkono.

Kupata zaidi juu ya hali ilivyo nimezungumza na Afisa wa Tume ya haki za binaadamu nchini Kenya Bw Hassan Omar Hassan, na kwanza nilimuuliza nini hasa la msingi lililotajwa kuwa ndiyo sababu ya kuwatia nguvuni wabunge hao.

Wabunge hao watatu na mwanaharakati Christine Nyagitha wote wameachiwa kwa dhamana leo baada ya kufikishwa mahakamani ambapo walikana mashtaka dhidi yao.

Hassan Omar (Kenya Human rights Commssion)

Mpitiaji:Josephat Charo