1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanariadha wengine watano wa Afrika wametoweka Gold Coast

12 Aprili 2018

Wanariadha 5 kutoka Rwanda na Uganda wanaaminika kutoweka, siku moja tu baada ya wengine wanane kutoka Cameroon kupotea

https://p.dw.com/p/2vuWE
Australien: Gold Coast Logo Commonwealth Games
Picha: gc2018.com

Waandalizi wa mashindano ya Jumuiya ya Madola wamesema wanariadha wengine watano wa Afrika wametoweka baada ya washiriki wanane kutoka Cameroon kupotea siku ya Jumatano.

Waandalizi wa mashindano hayo yanayofanyika mjini Gold Coast, Australia wamethibitisha ripoti kuwa wanariadha kutoka Rwanda na Uganda wanaaminika kupotea na pia wanawatafuta wachezaji wawili kutoka Sierra Leone.

Mkurugenzi mkuu wa shirikisho la mashindano ya Jumuiya ya Madola David Grevemberg amewaambia wanahabari kuwa wana wajibu kuhusu watu waliopata kihalali visa za kuwa Australia na mpaka pale watapopitiliza muda wa kukaa nchini humo ambao ni tarehe 15 mwezi ujao, wataendelea kutathmini hali.

Waziri wa mambo ya ndani wa Australia Peter Dutton ameonya kuwa wanariadha wataondolewa kwa nguvu nchini humo iwapo watajaribu kupitiliza muda walioruhusiwa kuizuru nchi hiyo. Mwaka 2000, zaidi ya wachezaji 100 walipotea katika mashindano ya Olimpiki ya Sydney.