Wanaofaidika nani na vita hivi vya sasa Mashariki ya kati? | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Wanaofaidika nani na vita hivi vya sasa Mashariki ya kati?

Jumuia ya kimataifa inapaswa iingilie kati haraka kuepusha balaa lisitaspakae Mashariki ya kati

Bomu la Israel lapiga kaskazini mwa Gaza

Bomu la Israel lapiga kaskazini mwa Gaza


Israel inaendelea kulishambulia eneo la Gaza tangu siku tatu zilizopita.Idadi ya waliopoteza maisha yao inazidi kuongezeka,ulimwengu wa kiarabu umeghadhibika.Eti kweli hiyo ndiyo njia ya kuwashinda nguvu Hamas?


Mwenyekubeba dhamana ya balaa lote hili linaloisibu Gaza,ni Hamas tuu.Kwa kuamua kusitisha makubaliano ya kuweka chini silaha,siku tisaa zilizopita na kwa kuanza upya kuvurumisha makombora dhidi ya maeneo wanakoishi watu nchini Israel,wamesababisha hujuma za kijeshi dhidi ya Gaza.Wamechochea makusudi hata kama wakati na kipeo cha mashambulio yenyewe vimewashangaza wengi tuu.


Bila ya shaka yoyote,Israel ina haki ya kujihami,raia wake wanaposhambuliwa.Watu hawezi pia kuitegemea Israel iwahurumie wanaharakati wa kundi ambalo,kwa wingi wao wanaendelea kupinga haki ya kuwepo dola ya Israel na kutumia nguvu pia dhidi ya dola hiyo.Lakini kila dola ya kidemokrasi inabidi ijitofautishe kikamilifu na wapinzani kama hao,kwa kuhakikisha raia wasiokua na hatia hawaangukii mhanga wa mashambulio ya kijeshi.Ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa na picha za televisheni kutoka Gaza zinabainisha walakin kataika matumizi ya nguvu.Kuwanusuru wasiokua na hatia wanaoishi katika eneo la msongomano la Gaza,ingawa si rahisi kwasababu Hamas wamejenga vituo vyao vya uongozi katika maeneo wanakoishi raia.Lakini suala linalozuka ni jee watu wamejaribu kweli kuwanusuru raia wasiokua na hatia?Na jee Israel inakadiria kwa namna gani ufanisi wa opereshini zake za kijeshi?


Kindani ndani Israel ndio itakayokula hasara.Ghadhabu katika nchi za kiarabu kutokana na namna damu inavyomwagika zinazidi kuongezeka kila hujuma zinapoendelea na kuwadhoofisha wote wale wanaopendelea amani pamoja na Israel.Balaa kubwa zaidi linaweza kuzuka:Wanamgambo wa Hisbollah nchini Libnan wamewekwa katika hali ya tahadhari.Iran imeshasema inawaunga mkono.Jumuia ya kimataifa haistahiki kuachilia watu wakiendekea kuuwawa na kusababisha balaa katika eneo zima la mashariki ya kati.

Inabidi ifanye kila liwezekanalo kuzilazimisha pande zote mbili zikubali haraka kuweka chini silaha.


Kimoja lazma Israel ikitambue:Hamas wataendelea kwa njia moja au nyengine kua hatari,hata kama wamedhoofika hivi sasa.Huenda hata wakapata nguvu zaidi kutokana na matukio haya ya sasa na kujipatia waafuasi zaidi hata katika maeneo ya ukingo wa magharibi.Hasara ya maisha na miundo mbinu,au hata kuteketezwa uongozi wao huko Gaza,yote hayo,wanaweza Hamas angalao kwa mtazamo wa muda mrefu,kuyavumilia.Kitu pekee ambacho pengine kinaweza kuwadhuru,ni kuwarahisishia hali ya maisha wapalastina na kufikia ufumbuzi wa mzozo wa mashariki ya kati,utakaokubalika kwa pande zote.

 • Tarehe 29.12.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GOm9
 • Tarehe 29.12.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GOm9
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com