1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanane wauawa Marekani katika shambulizi la risasi

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXiG

OMAHA.Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 amewaua watu wanane baada ya kufyatua risasi katika duka kubwa lililojaa watu waliyokuwa wakinunua vitu kwa ajili ya sikukuu ya Krismas nchini Marekani.Kijana huyo naye alijiua.

Polisi wa mji wa Omaha wanasema kuwa kijana huyo Roberts Hawkins aliwahi kukamatwa katika siku za nyuma kwa tuhuma za uhalifu pamoja na ulevi.

Katika shambulizi hilo watu watano wamejeruhiwa huku watatu wakiwa katika hali mbaya.

Rais George Bush alikuwa mjini humo saa chache kabla ya tukio hilo katika mkutano wa kuchangisha fedha za kampeni za chama chake cha Republican, alielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo.