1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo waripua vituo vya kupigia kura Pakistan

16 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D8Ut

ISLAMABAD:

Vituo vitatu vya kupigia kura vimeripuliwa Kaskazini-Magharibi ya Pakistan.Hakuna aliedai kuhusika na shambulizi hilo lakini inashukiwa kuwa ni wanamgambo wa itikadi kali za Kiislamu walio katika eneo hilo la machafuko karibu na mpaka wa Afghanistan. Mashambulizi hayo yamezusha hofu kubwa kuhusu usalama wakati wa kufanywa uchaguzi hapo siku ya Jumatatu.Kiasi ya wanajeshi 81,000 wamesambazwa kote nchini na hasa katika maeneo ya mivutano.