1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wa itikadi kali wa IS wabanwa Kobane

16 Oktoba 2014

Marekani inasema imewauwa "mamia kadhaa" ya wanamgambo wa itikadi kali wa dola la Kiislam IS katika mji wa Kobane, ingawa inakiri mji huo unaweza kuangukia mikononi mwa waasi hao wanaosonga mbele pia nchini Iraq.

https://p.dw.com/p/1DWP9
Hujuma za madage ya nchi shirika dhidi ya IS huko KobanePicha: Gokhan Sahin/Getty Images

Mshauri wa Marekani,jenerali mstaafu John Allen aliyerejea kutoka ziara ya Mashariki ya kati iliyokuwa na lengo la kuimarisha ushirika wa kimataifa dhidi ya wanamgambo wa IS,ameungama opereshini za kijeshi na hujuma za madege ya kivita hazitoshi kuwavunja nguvu wanamgambo wa IS.

Wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon inazungumzia kuhusu "mamia "ya wanamgambo wa itikadi kali waliouliwa katika hujuma za mabomu katika mji wa Kobane-mji wa Syria ulio karibu na mpaka wa Uturuki ambako vikosi vya wakurd vinapigana pia na wanamgambo hao wa madhehebu ya sunni.

Kwa mujibu wa uongozi wa kijeshi wa Marekani jeshi la Marekani kuanzia jumanne na jana jumatano limefanya hujuma mara 18 dhidi ya vituo vya wanamgambo wa IS huko Kobane na kwa namna hiyo kuwazuwia wasiendelee kusonga mbele.

"Lakini Kobane unaweza kutekwa" ametahadharisha msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon,John Kirby.

Wanamgambo hao wa itikadi kali wa IS wanasemekana kudhibiti takriban nusu ya mji huo wanaopanga kuutenga kabisa na sehemu nyengine ya dunia.

Kwa mujibu wa shirika linalosimamia masuala ya haki za binaadam nchini Syria,wapiganaji wa kikurd wamefanikiwa hata hivyo kuviteka vituo viwili kaskazini ya mji huo hapo jana.

Hujuma zaidi za nchi shirika zinahitajika

Shirika hilo lenye makao yake nchini Uingfereza limesema wanamgambo zaidi ya 600 wa IS wameuliwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, na wanajeshi wa kikurd katika mapigano ya nchi kavu katika mji huo.

Kämpfe um Kobane 16.10.2014
Moshi unafuka toka mji huo wa Syria ulioko Karibu na mpaka na UturukiPicha: Reuters/Kai Pfaffenbach

Maafisa wa kikurd wamethibitisha ripoti kwamba hujuma za madege ya kivita ya Ushirika unaoongozwa na Marekani zimesaidia kuwarejesha nyuma wanamgambo wa IS.

Hujuma zaidi za madege ya kivita ya nchi shirika zinahitajika,sawa na zinavyohitajika silaha na risasi zaidi kuendeleza mapigano ya nchi kavu dhidi ya IS amesema afisa mmoja wa kikurd ,Idriss Nassem katika mahojiano ya simu na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Uturuki ambayo ni mwanachama wa jumuia ya kujihami ya NATO imetuma wanajeshi,vifaru na mizinga karibu na mpakani lakini mpaka sasa haijaingilia kati.

Wakimbizi wamekwama katika eneo hilo la mpakani

UturukiiIlitajariwa pia kuruhusu madege ya kivita ya Marekani kuendesha opereshini zake toka ardhi ya nchi hiyo,lakini waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema wakimbizi wa Syria tu ndio wanaoweza kuvuka mpaka kwenda kuuhami mji wa Kobane.,akipinga wakati huo huo wito wa nchi za magharibi wa kufungua mipaka ya nchi hiyo.

Kobane Kämpfe Kurden Flüchtlinge IS
Wakimbizi wa Kikurd wanasimulia yanayojiri katika viwanja vya vita huko KobanePicha: DW/K. Sheikho

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu