Wanajeshi zaidi wa UA wawasili Moheli Comoro | Habari za Ulimwengu | DW | 21.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wanajeshi zaidi wa UA wawasili Moheli Comoro

FOMBONI:

Wanajeshi zaidi wa kikosi cha Umoja wa Afrika wamewasili katika kisiwa cha Comoro cha Moheli tayari kwa uvamizi wa kisiwa kilichoasi cha Nzuwani.

Wanajeshi hawa wanajumuika na wenzao wa jeshi la Comoro ambao walitangulia katika kisiwa hicho.

Wanajeshi 150 wa Tanzania wamewsili leo asubuhi katika bandari ya kisiwa cha Moheli ya Fomboni. Duru za kijeshi la Comoro zinasema kuwa wanajeshi zaidi wa Umoja wa Afrika wanatarajiwa kuwasili huko ijumaa jioni.

Kikosi cha kwanza cha Umoja wa Afrika cha wanajeshi 200 wa sudan na wengine 150 wa Tanzania kiliwasili huko alhamisi .Kisiwa cha Moheli ni moja wa visiwa vitatu vya Comoro.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com