Wanajeshi, waandamanaji Sudan waahidi kutekeleza makubaliano
8 Agosti 2019Naibu waziri wa masuala ya kisiasa nchini Marekani David Hale, amesema jana kuwa majenerali wa kijeshi wanaoongoza nchini Sudan pamoja na viongozi wa waandamanaji wametoa ahadi thabiti za kuingia katika kipindi cha mpito kurejesha mamlaka kwa uongozi wa kiraia.
Hale amesema hayo baada ya kukutana na kiongozi wa baraza la kijeshi; Abdel Fattah al- Burhan, viongozi wa waandamanji na maafisa wa vyama vya kijamii.
Baraza la kijeshi linaloongoza na viongozi wa vuguvugu la maandamano nchini humo walitia saini maazimio siku ya Jumapili yanayotoa njia ya kurejeshwa kwa mamlaka kwa uongozi wa kiraia baada ya zaidi ya miezi saba ya maandamano na ghasia.
Akiwahutubia wanahabari wakati wa mkutano mjini Khartoum, alipongeza mkataba huo, ulioongozwa na Ethiopia na Muungano wa Afrika na kuutaja kuwa wakihistoria.