1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli hiyo imewabeba wanaharakati na misaada kwa Wapalestina.

5 Juni 2010

Maandamano katika miji mingi duniani yafanyika kupinga hatua ya Israel ya kuzuia meli kuelekea Gaza.

https://p.dw.com/p/Nj4w
Mbinyo ya kimataifa dhidi ya Israel kulegeza sheria ya kuzuia usafiri katika eneo la Gaza, yazidiPicha: dpa

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wameingia ndani ya meli ya misaada ya Ireland inayoelekea Gaza baada ya kuizuia katika eneo la mpaka wa majini wa kimataifa. Msemaji wa jeshi hata hivyo amesema hakukuwa na mvutano na kulikuwa na ushirikiano kutoka kwa mabaharia na abiria.

Awali wanajeshi wa Israel walikuwa wametishia kuingia katika meli hiyo inayosafirisha misaada na wanaharakati ikiwa haingebadilisha mkondo wa kuelekea Gaza.

Schiff "Dignity" der Free Gaza Bewegung
Wanajeshi wa Israel washika doria kulidhibiti eneo la ukanda wa Gaza.Picha: picture-alliance/ dpa

Mapema wiki hii watu tisa waliuawa wakati wanajeshi wa Israel walipoingia katika meli ya Uturuki iliyokuwa imebeba misaada kwa ajili ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Jana kulikuwa na maandamano katika nchi za Kiarabu yakiitaka Israel iondoe sheria ya kuzuia usafiri katika ukanda ilioanza kutekelezwa baada ya kundi la Hamas kulidhibiti eneo hilo mwezi Juni mwaka wa 2007.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayesimamia haki za binaadam, Navi Pillay aliitaja hatua hiyo kuwa sio halali akisema sheria ya kimataifa inayolinda ubinadamu inapinga kuwanyima chakula raia kama mbinu ya kivita. Pillay pia alisisitiza kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya uvamizi wa Israel kwa msafara wa meli hizo.

Mwandishi, Peter Moss /DPA/RTRE

Mhariri, Mohamed Dahman