Wanafunzi wanahofia usalama wao Pakistan | Masuala ya Jamii | DW | 22.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Wanafunzi wanahofia usalama wao Pakistan

Hofu ya hali ya usalama imetandanda miongoni mwa wanafunzi wa shule katika eneo la kaskazini mwa Pakistan.

Pakistan Trauer nach Taliban-Überfall auf Schule in Peshawar 16.12.2014

Wanawake wakiwa katika maombolezo ya mkasa uliosababisha vifo vya wanafunzi wengi nchini Pakistan

Imetimia miezi 7 tangu kundi la watu wenye silaha kuivamia shule moja ya umma ya kijeshi katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa huko kaskazini mwa Pakistan, kuwauwa watu 145 wakiwemo wanafunzi 132. Kwa kiasi kikubwa kumbukumbu ya mkasa imetokea katika vichwa vya habari vya vyombo vya habari vya kimataifa, lakini familia za waathirika na manusura wa mkasa, kumbukumbu ya mkasa huo bado ipo kichwani kama ilivyokuwa siku ya tukio lenyewe. Akizungumza na shirika la habari la IPS akiwa nyumbani mjini Peshawar, mji mkuu wa jimbo la Khyber Pakhtunkhwa na ndilo hasa eneo la mkasa wa mwaka jana, Shahana Khan anashindwa kujizuia kububujikwa na machozi.

Kifo cha kusikitisha mtoto Asfand

Pakistan Trauer nach Taliban-Überfall auf Schule in Peshawar 16.12.2014

Wanafunzi wakiomboleza vifo vya wenzao nchini Pakistan

Mtoto wake mwenye umri wa miaka 15, Asfand, akiwa darasa la 10, alikuwa mmoja kati ya watoto wengi waliouwawa na kundi la Tahreek-e-Taliban Pakistan. Katika mkasa uliotokea Desemba 16, 2014. Nikimunukuu hapa mama huyo alisema" Tangu alipofariki, hapa nyumbani kumepooza kabisa", Asfand alikuwa mwenye kupenda dhihaka na kusababisha kicheko, lakini sasa ametuacha, hatuna lakusema".

Dada yake wa umri wa miaka 11 na mdogo wake wa miaka saba wamekuwa na hisia hizo hizo. Kama ilivyo kwa watoto wengine wanaoishia katika majnaga wanaonekana wakubwa zaidi ya umri wao wa kawaida.

Walikumbuka baadhi ya vichekesho vitimbi vilivyokuwa vikitolewa na ndugu yao, katika wakati ambao hawawezi kusahau baadae walianza kukububujikwa na machozi. Pamoja na yote hayo si mtoto wala mzazi aliyeitaja shule ambayo mauwaji hayo yalitokea, ingawa ilifunguliwa kiasi cha mwezi mmoja tu, baada mkasa huo kutokea.

Hali duni ya kiwango cha elimu

Kwa miezi kadhaa, familia nyingi zimekuwa katika hofu kubwa ya kurejea kwa mkasa ule. Pamoja na wanafunzi kuanza kurejea darasani hatua kwa hatua lakini wogo umetanda kila mahali. Hali hiyo ya mashaka yenye kuvuruga akili za wanafunzi wengi kwa wakati huu imekuwa moja kati ya vikwazo kwa serikali ya Pakistani yenye kutatiza ukuaji wa elimu katika taifa hilo lenye watu milioni 182.

Kwa kuzingatia Malengo ya Melenia, mpango wa Umoja wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na umasiki ulizinduliwa mwaka 2000, Pakistan imekuwa imekuwa nyuma ya mataifa mwengi wanachama.

Mwezi Machi wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilichapisha takwimu za mwaka 2013/2014, ambazo zilionesha kwamba serikali serikali haiwezi kufikia lengo la pamoja la kufanikisha elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2015, pamoja na uwepo wa ahadi nyingi katika makaratasi.

Sekta ya elimu nchini Pakistan inajumuisha zaidi ya shule 260,00o zikiwemo za serikali na binafsi, ambapo walimu milioni 1.5 wanawafundisha takribani wanafunzi milioni 42.9 nchini kote.

Kwa mujibu wa ripopti ya mwaka ya elimu ya Pakistan, iitwayo Pakistan Education for All 2015, ilitolewa pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kuna zaidi ya watoto milioni 6.7 ambao hawapati masomo, ikiwa moja katika viwangi vya juu kabisa vya watoto walio nje ya darasa duniani.

Ripoti inaonesha pia kiasi ya watoto milioni 21.4, wenye umri wa kwenda shule, ambao wanaandikishwa shule za msingi za serikali na binafsi ni asilimia 66 ndio wenye kufikia darasa la tano, na wengine asilimia 33.2 wanaacha kabla ya kumaliza elimu ya msingi.

Wataalamu wanasema kuondoshwa kwa mpango wa elimu ya taifa katika maeneo tete huko katika majimbo ya kaskazini ndiko kulikosababisha vikwazo katika ukuaji wa elimu.

Mwandishi:Sudi Mnette IPS
Mhariri:Josephat Charo

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com