Wanafunzi wafyatuliwa risasi Chuo Kikuu nchini Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wanafunzi wafyatuliwa risasi Chuo Kikuu nchini Marekani

CHICAGO:

Watu 5 wameuawa na 18 wamejeruhiwa katika ufyatuaji wa risasi uliotokea katika Chuo Kikuu kimoja karibu na mji wa Chicago nchini Marekani.Miongoni mwa waliofariki ni mshambuliaji aliejipiga risasi mwenyewe.Inasemekana kuwa kijana huyo mzungu alikuwa na bastola na bunduki inayopiga risasi kwa mfululizo na aliwalenga wanafunzi katika ukumbi wa mihadhara katika Chuo Kikuu cha Illinois ya Kaskazini.Watu wengi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu hospitalini.Baadhi yao wana majeraha mabaya vichwani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com