Wanafunzi wa vyuo vikuu DRC waandamana | Matukio ya Afrika | DW | 27.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Wanafunzi wa vyuo vikuu DRC waandamana

Polisi nchini Jamhuri ya Kidmokrasia ya Kongo wanapiga doria kwenye Chuo Kikuu cha Kinshasa kuwazuia wanafunzi wanaopinga kupandishwa kwa ada ya mtihani kutoka dola 5 za Kimarekani hadi 15.

Wanafunzi wa Institut National de Preparation Professionnelle nchini DRC

Wanafunzi wa "Institut National de Preparation Professionnelle" nchini DRC

Vurugu za wanafunzi zimesababisha uharibifu chuoni hapo, ukiwemo kuvunjwa kwa vyoo vya ofisi ya chuo na magari ya walimu. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia, mtu mmoja ameuawa, lakini Polisi wamekanusha, wakisema watu wamejeruhiwa tu, kama inavyosema ripoti ya Saleh Mwanamilongo aliyeko Kinshasa

Ripoti: Salehe Mwanamilongo
Mwandishi: Aboubakary Liongo
Mhariri: Othman Miraji